Jumatano 4 Februari 2026 - 09:00
Onyo kuhusu ongezeko la vurugu zisizo na kifani za Israel katika vita vya kimya kimya vinavyo endelea Ukingo wa Magharibi

Hawza/ Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetoa onyo kwamba Ukingo wa Magharibi unashuhudia “vita vya kimya kimya” na kiwango cha vurugu ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kinachotekelezwa na jeshi la Israel pamoja na walowezi.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa UNRWA, amesema kupitia akaunti yake binafsi kwamba; makumi ya maelfu ya watu, mwaka mmoja baada ya kuanza kwa operesheni ya Israel iitwayo “Ukuta wa Chuma”, wamekumbwa na kiwango kikubwa zaidi cha kuhama kwa lazima tangu mwaka 1967.

Mnamo tarehe 21 Januari, jeshi la Israel lilianzisha shambulio kubwa la kijeshi lisilo la kibinadamu kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, ambalo limesababisha vifo vingi pamoja na maelfu ya watu kujeruhiwa na kulazimika kuhama makazi yao.

Lazzarini alisema kuwa zaidi ya Wapalestina 1,000 wameuawa katika Ukingo wa Magharibi tangia Oktoba 2023, ambapo takribani robo yao ni watoto.

Aliongeza kuwa; mashambulizi ya walowezi wa Israel yanaendelea bila kukoma; wanawatisha na kuwaogopesha watu wa Palestina kila mara, wanawaua, wanaharibu vyanzo vyao vya maisha, na kutekeleza vitendo vya kikatili.

Rais wa UNRWA alisisitiza kuwa; shirika hilo linaendelea kutekeleza jukumu muhimu katika kutoa misaada ya dharura katika Ukingo wa Magharibi, “licha ya changamoto kubwa zilizopo”.

Chanzo: TRT WORLD

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha